Ijumaa, 25 Oktoba 2013

Una habari?


 
UPENDO NA FURAHA MINISTRY ni Huduma ya Kikristo inayo jihusisha na uponyaji kwa njia ya vyakula-lishe na miti-dawa. Huduma inatangaza nafasi za MAFUNZO YA UANDAAJI WA VYAKULA- LISHE MAALUMU KWA WAGONJWA WA PRESHA, KISUKARI, WATU WANENE NA WAATHIRIKA WA V.V.U.

Ada ya mafunzo ni SHILINGI ELFU ISHIRINI NA TANO TU ( Tshs. 25,000/-). Wahitimu wa mafunzo haya watapata nafasi ya kazi ya kuwahudumia kwa njia ya kuwaandalia vyakula-lishe wagonjwa mbalimbali wanao hudumiwa na huduma yetu waliopo katika mkoa wa Dar Es salaam.

MWOMBAJI AWE NA SIFA ZIFUATAZO

i. Umri miaka 16 hadi 45.

ii. Awe na elimu ya kuanzia darasa la saba hadi kidato cha nne.

iii. Awe mkristo aliye okoka na mwenye hofu kuu ya Mungu.

iv. Awe mkazi wa Dar Es salaam.

v. Awe na wito wa kazi ya kuwahudumia wagonjwa .

vi. Awe tayari kufanya kazi ya kuwahudumia kwa njia ya kuwaandalia vyakula-lishe, wagonjwa mbalimbali waliopo majumbani kwa muda wa miezi tisa kuanzia tarehe 02 Desemba 2013.


Mwisho wa kujiandikisha kwenye mafunzo haya ni tarehe 09 Novemba 2013.

Mafunzo yataanza tarehe 11 Novemba 2013 hadi tarehe 16 Novemba 2013.

Tunapatikana TABATA -KIMANGA kwenye kanisa la GOSPEL HEALING MINISTRY chini ya Mchungaji, Celestine Kalebi.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu 0784406508. Au tembelea upendonafuraha.blogspot.com


Source: http://www.wavuti.com/opportunities.html#ixzz2in4OZ2BN

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni