0/08/2013
Kampuni ya Neema Herbalist yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam, imejipanga kutengeneza fursa za ajira kwa vijana wasio kuwa na ajira waliopo katika wilaya mbalimbali za Tanzania Bara.
Fursa hizo za ajira zitatengenezwa kupitia mradi wa HERE TANZANIA ambao ni kirefu cha HERBAL REMEDIES in Tanzania PROJECT. Mradi huu umelenga katika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa upandaji wa miti dawa na namna wanavyo weza kukitumia kilimo cha mitidawa kama chanzo cha kutengeneza kipato, pamoja na kuwahamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa matumizi ya dawa asilia. Mradi huu unaratibiwa na kampuni ya Neema Herbalist kwa kushirikiana na mashirika rafiki pamoja na wadau mbaimbali wanao jihusisha na masuala ya utunzaji wa mazingira.
Akizungumza na mwandishi wa makala haya, Mratibu wa mradi wa HERE TANZANIA, ndugu, Africanus N’gwalu, amesema kuwa lengo la mradi huu ni kupanda miti dawa ya aina mbalimbali ipatayo milioni tatu, ifikapo tarehe 30 NOVEMBA 2014 katika wilaya zote za Tanzania bara ambayo ni sawa na wastani wa miti elfu kumi na tano katika kila wilaya. Miti dawa itakayopandwa itakuwa ni miti yenye kutibu magonjwa mbalimbali yanayo mkabili mwanadamu kama vile vile kisukari, presha, ugumba, utasa, na nguvu za kiume kwa kutaja machache.
Zoezi hili litasimimamiwa na vijana wapato mia moja kutoka katika kila wilaya ya Tanzania Bara, ambao watapatiwa jukumu la kuwahamasisha wananchi kuhusu upandaji wa miti dawa mashambani na

majumbani pamoja na kuwahamasisha kuhusu umuhimu wa matumizi ya dawa asilia.
Katika kuhakikisha kuwa lengo hili linatimia kwa muda ulio pangwa, mradi umejipanga kutoa mafunzo ya wiki tatu kwa vijana wapatao mia moja katika wilaya zote za Tanzania bara, ili kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kama wasimamizi wa shughuli kuu za mradi katika wilaya zao kama vile kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kupanda miti dawahalikadhalika umuhimu wa matumizi ya dawa asilia.
Mradi huu ni matokeo ya utafiti ulio fanywa na kampuni ya Neema Herbalist kwa muda wa mwaka mmoja, kuanzia mwezi May 2012 hadi mwezi May 2013 kuhusu Umuhimu wa Matumizi ya Tiba Asilia kwa ustawi wa afya za wananchi pamoja na maendeleo ya sekta ya ujasiriamali nchini hususani kwa wajasiriamali waliowekeza ama wanao fikiria kuwekeza kwenye masuala ya tiba asilia. Matokeo ya utafiti huu yanaeleza kuwa kuna soko kubwa sana la mitidawa kutoka Tanzania, ndani na nje ya Tanzania (kimataifa) na hivyo kufanya hitaji la kuwekeza katika kilimo cha upandaji wa miti dawa kuwa kubwa sana.
Hitaji la kuwekeza kwa nguvu zote katika kilimo cha miti dawa linachangiwa na ukweli kwamba ni wakulima wachache sana nchini Tanzania au hakuna kabisa ambao wamewekeza kwenye kilimo cha upandaji wa miti dawa na badala yake wengi wao wameweka nguvu zao nyingi kwenye mazao mengineyo ya biashara na chakula huku wakilipa kisogo suala la kilimo cha miti dawa. Mbali na kutengeneza fursa nyingi za ajira kwa vijana watakao hamasishwa na kilimo cha miti dawa, kilimo cha miti dawa kitasaidia katika kuimarisha afya za watanzania kupitia matumizi ya miti dawa na hivyo kuchochea maendeleo ya jamii na taifa zima kwa ujumla.
Mradi umepanga kutoa mafunzo ya wiki tatu kwa vijana wapatao mia moja (100) kutoka katika kila wilaya ya Tanzania bara yatakayo wajengea uwezo wa kufanya kazi ya kuwahamasisha wananchi kuhusu upandaji wa miti dawa katika wilaya wanazoishi. Kwa uanza, tutaanza na kutoa mafunzo kwa vijana kutoka wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke. Baada ya mafunzo haya ya awali kwa vijana hawa, tutawagawanya katika makundi makuu mawili. Kundi la kwanza, tutawapeleka katika wilaya mbalimbali za Tanzania bara kwa ajili ya kwenda kutoa mafunzo waliyoyapata kwa vijana waliopo katika wilaya hizo, huku kundi jingine likiendelea na taratibu za awali za uhamasishaji kwa hapa jijini Dar es Salaam.
Baada ya vijana wa mikoani kupatiwa mafunzo, shughuli za uhamasishaji zitaanza rasmi nchi nzima, na zitafanyika kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia tarehe 02 Novemba 2013 hadi tarehe 30 Novemba 2014.
Kwa vijana waliopo mkoani Dar es salaam, fomu za kujiunga na mafunzo haya zitaanza kutolewa rasmi siku ya Jumatatu ya tarehe 12 AGOSTI 2013 katika ofisi zetu zilizopo katika eneo la CHANGANYIKENI karibu na CHUO CHA TAKWIMU. Mwisho wa kutoa fomu za kujiunga na mafunzo haya itakuwa ni tarehe 28 AGOSTI 2013.
Kwa maelezo zaidi kuhusu sifa na taratibu za kujiunga na mafunzo haya, tafadhali tembelea: www.neemaherbalist.blogspot.com

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/08/mradi-wa-upandaji-miti-dawa-kutengengeza-fursa-za-ajira.html#ixzz2biR4G5hl
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni