Jumapili, 11 Agosti 2013

Sijasema madawa ya asili, niliongelea upandaji miti


0/08/2013
 
Picture: Neema Herbalist
Kampuni ya Neema Herbalist yenye  makao yake makuu jijini Dar es Salaam, imejipanga kutengeneza  fursa za  ajira  kwa  vijana   wasio  kuwa na ajira waliopo  katika wilaya mbalimbali  za Tanzania Bara. 

Fursa hizo za ajira zitatengenezwa kupitia mradi wa HERE TANZANIA  ambao ni kirefu cha HERBAL REMEDIES in Tanzania PROJECT. Mradi huu umelenga katika kutoa elimu  kwa wananchi  kuhusu umuhimu  wa upandaji wa miti dawa na namna wanavyo  weza kukitumia kilimo cha  mitidawa  kama chanzo cha kutengeneza  kipato, pamoja na kuwahamasisha  wananchi kuhusu umuhimu  wa matumizi ya dawa asilia.  Mradi  huu  unaratibiwa na kampuni ya Neema  Herbalist  kwa kushirikiana na mashirika rafiki  pamoja na wadau  mbaimbali wanao  jihusisha  na  masuala ya utunzaji wa mazingira. 

Akizungumza  na  mwandishi  wa  makala  haya, Mratibu  wa  mradi  wa HERE TANZANIA, ndugu, Africanus  N’gwalu, amesema  kuwa lengo  la  mradi  huu  ni  kupanda miti  dawa ya  aina  mbalimbali  ipatayo  milioni  tatu, ifikapo  tarehe  30 NOVEMBA 2014  katika  wilaya  zote za Tanzania bara ambayo ni  sawa  na  wastani  wa  miti  elfu  kumi  na  tano  katika  kila wilaya. Miti dawa  itakayopandwa itakuwa ni  miti yenye kutibu  magonjwa  mbalimbali  yanayo  mkabili  mwanadamu  kama  vile vile  kisukari, presha, ugumba, utasa,   na  nguvu  za  kiume  kwa  kutaja  machache.

Zoezi  hili  litasimimamiwa  na vijana wapato mia  moja  kutoka  katika kila wilaya ya Tanzania  Bara, ambao  watapatiwa jukumu la kuwahamasisha wananchi  kuhusu  upandaji wa miti dawa mashambani na

majumbani  pamoja  na  kuwahamasisha  kuhusu  umuhimu wa matumizi ya dawa  asilia. 
 
Katika kuhakikisha  kuwa lengo hili  linatimia kwa  muda  ulio pangwa, mradi  umejipanga  kutoa  mafunzo  ya  wiki  tatu  kwa  vijana wapatao  mia  moja  katika   wilaya zote  za Tanzania  bara, ili kuwajengea  uwezo  wa  kufanya  kazi kama  wasimamizi  wa  shughuli kuu za mradi  katika  wilaya  zao  kama  vile  kuwaelimisha  na  kuwahamasisha  wananchi  kuhusu   umuhimu wa kupanda  miti dawahalikadhalika  umuhimu  wa  matumizi  ya  dawa  asilia. 

Mradi  huu  ni  matokeo ya  utafiti  ulio   fanywa  na  kampuni ya Neema  Herbalist  kwa  muda  wa  mwaka  mmoja,  kuanzia  mwezi  May  2012  hadi  mwezi  May  2013  kuhusu Umuhimu wa Matumizi ya Tiba  Asilia  kwa  ustawi  wa  afya  za wananchi  pamoja  na  maendeleo  ya  sekta ya  ujasiriamali  nchini  hususani  kwa  wajasiriamali  waliowekeza ama wanao  fikiria kuwekeza kwenye  masuala  ya  tiba  asilia. Matokeo  ya  utafiti  huu  yanaeleza  kuwa kuna  soko  kubwa  sana  la mitidawa kutoka Tanzania,  ndani  na  nje  ya  Tanzania (kimataifa) na  hivyo  kufanya  hitaji la kuwekeza katika  kilimo cha upandaji  wa  miti  dawa  kuwa  kubwa  sana.

Hitaji  la kuwekeza kwa nguvu zote  katika kilimo  cha  miti  dawa  linachangiwa  na  ukweli  kwamba  ni  wakulima wachache  sana  nchini  Tanzania  au  hakuna kabisa  ambao  wamewekeza  kwenye  kilimo  cha  upandaji wa  miti  dawa na badala yake  wengi wao wameweka  nguvu zao  nyingi  kwenye  mazao  mengineyo ya biashara na chakula huku wakilipa  kisogo  suala  la  kilimo  cha  miti  dawa.  Mbali  na  kutengeneza  fursa  nyingi za ajira kwa vijana watakao hamasishwa  na  kilimo  cha  miti  dawa,  kilimo  cha  miti  dawa  kitasaidia  katika  kuimarisha  afya za  watanzania kupitia  matumizi  ya  miti  dawa  na  hivyo  kuchochea  maendeleo ya jamii na taifa zima kwa ujumla.

Mradi  umepanga  kutoa  mafunzo ya wiki  tatu kwa vijana  wapatao  mia moja (100) kutoka katika  kila  wilaya  ya  Tanzania  bara  yatakayo  wajengea uwezo  wa  kufanya kazi  ya  kuwahamasisha wananchi    kuhusu  upandaji  wa  miti  dawa  katika  wilaya wanazoishi. Kwa uanza, tutaanza  na  kutoa mafunzo kwa  vijana  kutoka  wilaya  za  Kinondoni, Ilala na  Temeke. Baada ya  mafunzo  haya ya awali kwa vijana  hawa, tutawagawanya  katika  makundi  makuu  mawili. Kundi la kwanza, tutawapeleka  katika wilaya mbalimbali  za  Tanzania  bara  kwa  ajili  ya  kwenda   kutoa  mafunzo waliyoyapata  kwa vijana waliopo katika  wilaya  hizo, huku  kundi  jingine  likiendelea  na  taratibu za awali  za  uhamasishaji  kwa  hapa jijini  Dar es Salaam.

Baada ya vijana wa mikoani  kupatiwa mafunzo, shughuli za uhamasishaji zitaanza rasmi nchi nzima, na  zitafanyika  kwa muda wa mwaka mmoja  kuanzia tarehe  02 Novemba 2013 hadi tarehe 30 Novemba  2014.

 Kwa  vijana  waliopo mkoani  Dar es  salaam, fomu  za  kujiunga  na  mafunzo  haya  zitaanza  kutolewa  rasmi  siku  ya  Jumatatu  ya  tarehe  12  AGOSTI  2013   katika  ofisi  zetu  zilizopo  katika  eneo  la  CHANGANYIKENI  karibu  na CHUO CHA TAKWIMU. Mwisho wa kutoa fomu  za  kujiunga na mafunzo haya  itakuwa ni  tarehe 28 AGOSTI  2013.

Kwa  maelezo zaidi  kuhusu  sifa  na  taratibu  za  kujiunga  na  mafunzo  haya, tafadhali  tembelea: www.neemaherbalist.blogspot.com


Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/08/mradi-wa-upandaji-miti-dawa-kutengengeza-fursa-za-ajira.html#ixzz2biR4G5hl

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni