Naona fani zisizo na utaratibu wa practical training hapa UDOM tukiwasaidia kuwasiliana na NGOs pia mashirika mbalimbali ili wakajifanyie kazi za muda mfupi kwa ajili ya kujipatia ujuzi na uzoefu
Naona makampuni yakijitangaza kupitia blog hii
Naona wanafunzi wengi nje ya wanaCASFETA wakiomba kuungwa kwenye mtandao huu
Naona wanaCASFETA wakiwa wameungana na kufahamiana zaidi huko vijijini mwao wanakokuweko na hata kuunga nguvu za pamoja kwa ajili ya ukombozi wa kifikra hata kuleta badiliko la kweli kwenye nchi yetu
Naona kila kijiji kikiwa na mwanaCASFETA anayeitetea
Naona kata kikiwa na wanaCASFETA wanaoungana kusababisha nguvu ya badiliko
Naona wilaya ikiwa inafurahia baadhi ya wanaCASFETA walioungana kujenga taifa endelevu
Naona mikoa yote Tanzania ikitabasamu kwa ajili ya vijana waadilifu walio wanaCASFETA walioungana
Naiona Tanzania iliyokombolewa na wanaCASFETA
kuwa chanzo cha hii kuona kwangu kwa kushiriki kikamilifu kwenye blog hii, hebu tuifanye mashuhuri kwenye google uone nini kitatokea, usifanye kwa ajili yako mwenyewe bali kwa ajili ya mwanao atakayekuja kusoma UDOM hiyo miaka ijayo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni