Utangulizi
Kutoka mwaka 2011/12, kulionekana upungufu mkubwa sana kwa
wanafunzi (waliookoka) wanaohitimu kutojiandaa ama kutoandaliwa kuhitimu masomo
yao na kuingia mtaani kwa ajili ya kuyakabili maisha baada ya chuo. Tuligundua
watu wengi kutokuwa na maandalizi ya nyaraka muhimu kama vile CV na hata vyeti
kutokuwa katika mpangilio unaokubalika. Pia wahitimu wengi mbali na kujua
kutumia Internet kwa ajili ya kufanya kazi zao za darasani, imeonekana kuwa
hapo ndio mwisho wao – hawajui kuwa kazi zinaweza kupatikana humo, kujitolea, mawasiliano
na vitu vingine vingi. Wachache ambao tuliweza kuwaandaa kibinafsi mwaka huo,
waliingia mtaani kwa ujasiri na mpaka sasa wanafanya vizuri ila tukagundua pia
kuwa wahitimu wengi hawapo tayari kuambiwa jambo na mtu wa mwaka wa chini yao
na ili kukwepa tatizo hili, mbadala ulianza kutafutwa na ndiposa April 27 – 28,
2013 tukafanikiwa kuanzisha workshop moja iliyopewa jina la CCkwaCC workshop.
Ilitokeaje: Katika kutafuta namna gani angalau wanaCASFETA
wataweza kuwa na nuru watokapo kwenye maisha ya uanafunzi na kuyakabili maisha,
Samson J. (PSPA) amekuwa akibadilishana mawazo na watu mbalimbali, ndipo siku
moja uhakika wa upungufu mkubwa ulipodhihirika pale ambapo mashahidi wawili
Kaaya G. (BAGE) na Kyando N. (BAGE) walipothibitisha kuwa hii hali ikiendelea
kuachiwa hivi, hata ukombozi wa nchi yetu unaosemwa kila mara kuwa wanaCASFETA
wataikomboa nchi utaendelea kuwa mgumu. Samson huwa anaweza kuthubutu
kujaribisha jambo linaloonekana kuwa lingemfaidisha mtu mwingine huku yeye
akiendelea kujipatia uzoevu na ujuzi ambao unakuja tu kama utamshirikisha mtu
mwingine kile unachoona kuwa kisipokwepo kitasababisha upungufu unaopelekea
uharibifu.
Jioni moja baada ya ibada (April 5, 2013) hapa Common Room
ya Block 2, wahitimu wote waliombwa kubaki ili wauziwe maono, wote waliafiki na
kamati ndogo kuundwa ikimhusisha Rajabu R. (BAPA), Leonard P. (IR), Charles G.
(PHIL), Mfilinge M. (BAGE), Jonathan V. (EDM), Chisata D. (PPM&CD) na
Mwinuka M. (DS). Hii ni kamati ambayo ilikutana rasmi kwa mara ya kwanza April
9, 2013 na kuidhinisha baadhi ya mambo.
Wakati huo huo, Samson kwakuwa ni mobilizer mzuri pia,
alianza mchakato wa kukusanya emails za wahitimu na unakumbuka kuwa ndiye
alikuwa mwasisi wa a centralized base ya taarifa za wanaCASFETA. Hivyo kazi
ilikuwa rahisi zaidi.
Siku ya workshop ya kwanza, watu walifurahi sana na habari
zikaenea kwani Samson mwenyewe aliShare ‘What to do from today on until you are
employed’, Elisha D. (IR) akaShare ‘Forming business groups’, ‘Fund raising and
donors finding’, ‘Time management’ na mwisho kwa siku hizo mbili za kwanza ni
Mr. Magambo R. (Former UDOSO president na sasa ni Lecturer SJUT wakati huo huo
akimiliki kampuni yake) aliShare ‘Financial skills’.
Lengo: siku ifike ambayo pasipo kuhurumiwa wala kupendelewa,
mwanaCASFETA mmoja wetu astahili kuwa na wadhifa kwa ajili ya taifa letu – Dan
2:48
Kauli dira: kufaana sisi kwa sisi kwa kushirikishana ujuzi
na taaluma mbalimbali hata kutokeza fursa ya haki – Dan 2:49
Mengi yapo ya kusema ila kwa waraka huu, tulitaka tu
kuelezea malengo ya CCkwaCC Empowerment
1.
Kuwafundisha mwaka wa kwanza pindi tu wafikapo
hapa chuo habari ya bum, matumizi na financial skills kwa ujumla wake ili
a.
Waweze kuwa imara wasichukuliwe na ulimbukeni wa
kujishikia pesa zao wenyewe kwa mara ya kwanza na hivyo kutumia vibaya mpaka wanaishiwa
njiani
b.
Kuweka mipango ya kununua laptop badala ya simu
za gharama angalau ifikapo semester ya pili ya mwaka wa pili – tatizo kubwa
linalowakabili wanaCASFETA hapa chuo wafikapo mwaka wa mwisho ili kuandaa
nyaraka zao ni kutomiliki PC zao
c.
Kuwaelekeza washirika wetu waepuke kujiingiza
kwenye mahusiano ya kimapenzi kama hawajapanga kuoa. Kwenye CCkwaCC tunasema
‘mwambie mtu unampenda kama tu upo tayari kuolewa naye/kumwoa leo na ya kuwa
umeweka mpango kuwa upo tayari kuoa unapoenda kumwambia ama unapomkubalia
kumpenda’. Tuwaambie washirika wetu wajitahidi kuweka ukaribu na wazazi wao hasa
kwenye mambo haya ya kuoa na kuolewa. CCkwaCC huwa inashangaa mtoto wa
kike/kiume anapokuwa kwenye mahusiano mwezi mzima bila ya mama/baba kujua.
Kweli? Haikuandikwa wazazi ndiyo watu wa pekee wenye uwezo ku-Influence miaka
yako ya kuishi? Je, wajua kuwa wewe kuolewa/kuoa ni kumwongeza mtoto mwingine
kwenye familia ya wazazi wako? Iweje umlete mtoto mgeni ambaye hukuwahi hata
siku moja kuwadokezea wazazi wako kuhusu kumkubali kwako? Siku Samson anaenda
kuongea na huyu mwanamke mzuri leo, aliwaaga wazazi kuwa ‘naenda kumtongoza
dada nanii akubali nimwoe’
d.
Kuelimisha wanachama wetu kuhusu optional
courses, credits, supplementary, disco,
na mengine mengi ya kielimu hapa chuo – wengine wanaOpt kozi isiyo na mashiko
e.
Kuwapa mwaka wa kwanza walezi ambao ni mwaka wa
pili/tatu/nne wa kozi zao
f.
Upatikanaji na utunzaji wa taarifa muhimu za mwaka
wa kwanza kama vile room, block and phone number, degree program, full name,
kijiji na wilaya atokako(nyumbani), mchungaji wake huko alikotoka na hapa akiwa
chuo, na kama amebatizwa kwa maji mengi. Wapi anaenda wakati wa likizo hii na
wapi atakwenda baada ya kuhitimu degree yake hapa chuo. Kwa ujumla ni kuwa,
washirika wetu ni wale wanafunzi tu waliookoka na kubatizwa kwa maji mengi na
wanaabudu kwenye makanisa ya kiPentekoste lakini yenye wachungaji wa mahali
pamoja
g.
Muhimu sana: kuwahamasisha mwaka wa kwanza
washirika wetu watumie ile likizo ya wiki mbili ya semester ya kwanza kuandaa
CV ambayo itakuwa dira tayari kwa semester ya pili kulazimika wakajipatie
maeneo ya kufanyia practical training for experience (kwa kujitolea BURE ama
kulipwa ikitokea). Matatizo ni mengi kwa watu kutokuwa na ujuzi
h.
Kukazia usomaji kwa kutumia maarifa ili asiwepo
mwanaCASFETA anayeshindwa kuwepo ibadani kisa anasoma sana , nafikiri kuna
ushahidi wa baadhi ya watu walioDisko wakiwa washirika wanaCASFETA na walikuwa
adimu ibadani na bado wamedisko wakati wale waaminifu bado wamefadhiliwa na
Mungu.
i.
Kama zawadi hizi za kitaaluma huwa zinatolewa
kwa haki, basi safari hii tunazitaka, tuna uwezo na tumejipanga na Bwana
aridhie matakwa haya – ni ahadi yake pia
j.
Kuendeleza na kuhamasisha utumiaji wa computer
katika kuangalia fursa za scholarships, kazi, volunteering, taarifa za kiujuzi,
na kuwasiliana
k.
Elimu ya computer, hasa
i.
Emailing na matumizi ya soft ware mbalimbali –
skype, viber, ….pc suite, Encarta, typing game, …. – watu wenye simu zenye
internet sio wote wanatakiwa kununua modem, tuwaelimishe watu wetu
ii.
Ms word (HASA haya maeneo)
Spell checker; Referencing; Automatic table of content and cover page; Thesaurus;
Pagination; Watermarking; Finding and replacing within a whole document; Insertions
iii.
Ms excel
iv.
Ms access na publisher
v.
Ms outlook
vi.
Ms power point
2.
Baada ya kuweka huo msingi kwa mwaka wa kwanza,
sasa kazi inakuwa rahisi kwa miaka inayofuata kuwa ni mwendelezo tu kuweka
nguvu kwenye
a.
Kuwaelimisha washirika wetu wazijue degree zao
na kazi wanazopaswa/kuweza kufanya
b.
Kuwajengea uwezo waweze kujipatia marafiki
maeneo yote kuanzia kwa lecturers ili iwe rahisi wakati wa kuwatafuta referees
c.
Leadership skills kwa mapana yake - management vs administration
d.
Networking na watu mablimbali na mbinu hapa
itakuwa ni kutembelea maeneo mbalimbali kama bungeni, workshops nyingi,
kujiunga na organizations kama vile AIESEC, RestLess, BRAC, kuwa na email na
kutumia kuwasiliana
e.
Kuwaelekeza washirika wetu wawe msaada
makanisani mwao kwa wao kujitolea kutumia taaluma zao kuwaendeleza watu
wengine. Tunataka iwe, kanisa lolote lenye mwanaCCkwaCC basi watu wote
waliochini ya umri wa miaka 20 wajishugulishe kuwa na cheti cha form four kama
ilitokea hawana ili waweze kujiendeleza kielimu
f.
Kuwahamasisha na kuwaelimisha washirika wetu
wawe watu wanaotembea na mawazo ya kibiashara na waandike mawazo hayo huku
wakiangaza nani wa kushirikiana naye kwenye biashara yenyewe – waazishe NGO,
kampuni……. Tuwape elimu ya nini cha kuzingatia wakati wa kuwatafuta watu wa
kufanyanao kazi – taaluma inayohusika, sababu ya mtu kuhusishwa, uwezo wa
kuInfluence serikali/jamii, ……
g.
Kuelimisha washirika wetu waandike miandiko ya
miradi kwa ajili ya vijiji vyao
h.
Business partnership – hisa na kuingia ubia na
kampuni iliyotayari
i.
Uadilifu, kutunza muda na ubunifu (kujijengea
ubora) kwenye kufanya haya mambo yote madogomadogo ya kawaida ambayo watu
wengine huyafanya kwa kawaida
j.
Kuwajengea washirika wetu uwezo mkubwa wa Public
Speaking
k.
Fursa ya uongozi CASFETA iwe ni a field of
practice ya utumishi wa nchi
l.
Kujenga miundo ya lecturers wetu kukutana na
washirika wetu via academic presentations
m.
Utambuzi wa vyuo nchi nzima na kugawa majukumu
kwa wahitimu CCkwaCC iwe huko
n.
Kujiwekea akiba kubwa ya mtaji wa watu kwa
kufanya mazuri huko kote tunakopita kuanzia mwaka wa kwanza – watu ni zaidi ya
kuwa na hela nyingi za kufanyia utakacho
o.
Kuwakutanisha washirika wetu na makampuni
mbalimbali kwa kuwaalika ama kuwapeleka wakatembelee huko VODACOM, MADINI,
MANISPAA, TAMISEMI, …
p.
Kuelimisha namna ya kuandika ‘a current cover
letter, resume, CV, application letter, scanning documents, attractive emails……
q.
Kuwalekeza washirika wetu watume CV zao mwanzoni
mwa semester ya mwisho kwa mwaka wao wa masomo lakini wakielezea bayana siku
yao ya kuhitimu chuo
r.
Kuweka bayana kuwa tunataka ¾ ya wanaCASFETA
wawepo serikalini (watumishi waadilifu sana) lakini wakati uo huo kila mmoja
akiwa na kitu anachokifanya nje ya ajira ya serikali – kuwepo serikalini ni
fursa ya soko la biashara yako, fursa ya kufahamiana na watu, fursa ya
security, fursa ya mtaji, ….
3.
Namna ya kufanya
a.
kuShare, sisi kwa sisi, yaani kila mmoja wetu
mwenye kujua jambo fulani, ashirikishe
b.
kuwaalika watu nje ya chuo ili kushirikisha
c.
kufuatilia na kusimamia impacts ya kila sharing
iliyotolewa – hasi kudhibitiwa na chanya kuendelezwa
d.
kuwa na mikutano ya mara kwa mara kwa ajili ya
tathmini ya nini kilijiri/kifuate
e.
mwanzoni mwa semester kabisa, kupanga na
kujulisha kanisa kuhusu ratiba za CCkwaCC Empowerment ili ikitokea imegongana
na ratiba ya kanisa, ihamishwe ya CCkwaCC na sio kuahirishwa – Setting
objectives and action plans is a must in every year
f.
kufuatilia wahitimu wote wa mwaka uliopita kama
wako wapi na wanafanya nini
g.
kuwaunganisha wahitimu wa mwaka huu na wale wa
mwaka uliopita huko ‘mawilayani’ ama majumbani kwao
h.
kutunza kumbukumbu ya wahitimu na washirika wote
kwenye hardcopy na softcopy – mfano upo kwenye nyaraka za Samson
i.
kuchagua uongozi kabla ya UE ya semester ya
mwisho wa mwaka wa masomo
j.
kuwa na kamati ndogondogo kila inapohitajika –
uwiano wa kozi utazingatiwa
4.
Waendelezaji wa CCkwaCC Empowerment hapa CHSS
mwaka 2013/14
JINA KAMILI
|
SIMU
|
KOZI
|
YoS
|
SKULI
|
E MAIL
|
NYUMBANI
|
MARKO TIMOTHY
|
0762 187615
|
BASO
|
II
|
SS
|
|
Iramba
|
JUSTINE SAMSON
|
0768 338434
|
PSPA
|
-
|
SS
|
justinesamson34@yahoo.com
|
Monduli
|
MASSE DANIEL
|
0764 929637
|
BAGE
|
III
|
SS
|
massed89@gmail.com
|
Karagwe
|
JULIAN EMMANUEL
|
0765 257615
|
DS
|
III
|
SS
|
|
|
ANTHONY LEVINA
|
0714 992735
|
BBA
|
III
|
SH
|
|
|
OSWARD BADI
|
0766 241723
|
BCOM PLM
|
II
|
SH
|
|
|
FRANK KIGOYE
|
0712 315087
|
BCOM IB
|
II
|
SH
|
|
|
DANIEL THOBIAS
|
0765 294886
|
BA ENG
|
II
|
SH
|
|
|
ERASI EMMANUEL
|
0759 844364
|
Bsc CoEng
|
-
|
CIVE
|
myesierasi@yahoo.com
|
|
MATHIAS JAMES
|
0752 293434
|
LLB
|
II
|
SH
|
|
|
5.
Msimamo wetu
a.
Hata ijapokuwa tunafanya vitu ambavyo
vinawezakumsaidia mtu aliye kiroho kuwa bora zaidi, hatuko kidini na hatufanyi
chochote ambacho ni kinyume na maadili ya chama kinachotuweka pamoja kama
wanafunzi tuwapo hapa chuo
b.
Wala hatuna na hatutaandaa ratiba
zinazojitegemea nje ya chama chetu cha wanafunzi na kwahiyo, uongozi wa chama
husika hapo tulipo unao uwezo wote kutuelekeza namna gani tuboreshe shughuli
zetu na hata hivyo nakala ya mwongozo na ratiba zetu lazima katibu mkuu wa tawi
letu awe nayo. Kiongozi mmoja mstaafu tawini ni mwanakamati wa tume ya
kuendeleza CCkwaCC Empowerment – kamati kuu ya tawi kwa hiari ama kwa maombi
yetu watamwidhinisha mmoja wao atakayekuwa mwanakamati
6.
Mwisho
Mungu
ibariki CASFETA ya Social Science – UDOM ili siku moja kupitia CCkwaCC
Empowerment imtoe kiongozi mkubwa wa nchi hii, Mungu wabariki waasisi wa
CCkwaCC, Mungu Ibariki Tanzania na ibariki Africa ambayo siku moja itakuwa
ikiendesha CCkwaCC Empowerment kwa ajili ya kuwatoa wanafunzi bora waliookoka
wenye elimu ya kutosha ya uraia kiasi cha kutofautisha siasa na ukombozi wa
nchi zao. Siasa ina mbadala (pesa, nguvu, nafasi, umashuhuri n.k.) lakini
ukombozi wa nchi ni wenyewe tu kuwa ni “wananchi watengwe mbali na wale maadui
wakubwa wa nchi zetu ambao ni umaskini, ujinga na magonjwa”. Ni ujinga ndiyo
unaoleta ubaguzi wa kidini, ni kiwango cha umaskini ndiyo unawafanya watu
waandamane wiki nzima. Ni umaskini ndiyo unaoifanya serikali isijali maslahi ya
wananchi wake na kupelekea wananchi waandamane kwa sababu viongozi wao
wamejiwekeza kwenye kujali maslahi yao pekee
Imeandaliwa na Samson J. (PSPA) ______________
Mwasisi wa wazo
Na kusomwa/kuhaririwa na wafuatao ambao walikuwa ni kamati ya kwanza
kabisa ya CCkwaCC
1.
Rajabu
R. (BAPA)___________________,
2.
Leonard P. (IR)_____________________,
3.
Charles G. (PHIL)___________________,
4.
Mfilinge M. (BAGE)_________________,
5.
Jonathan V. (EDM)__________________,
6.
Chisata D. (PPM&CD)____________ ____na
7.
Mwinuka M. (DS) _____________________.
Na
kuridhiwa/kuidhinishwa na viongozi wetu wa CASFETA Social Science – UDOM
2012/13
1.
Mwenyekiti _______________ Julian Emmanuel (DS)
2.
Katibu __________________Fabian Bernard
(PPM&CD)
Toa mawazo yako ili cckwacc iendelee kuwepo ikiwa bora na wewe ukiwa mdau mkuu ukiendelea kushiriki kuboresha
JibuFuta