Jumatatu, 24 Juni 2013

Blog ya CCkwaCC


blog inakuja, imeelekea kukamilika

historia fupi ni kama ifuatavyo

Kutoka mwaka 2011/12, kulionekana upungufu mkubwa sana kwa wanafunzi (waliookoka) wanaohitimu kutojiandaa ama kutoandaliwa kuhitimu masomo yao na kuingia mtaani kwa ajili ya kuyakabili maisha baada ya chuo. Tuligundua watu wengi kutokuwa na maandalizi ya nyaraka muhimu kama vile CV na hata vyeti kutokuwa katika mpangilio unaokubalika. Pia wahitimu wengi mbali na kujua kutumia Internet kwa ajili ya kufanya kazi zao za darasani, imeonekana kuwa hapo ndio mwisho wao – hawajui kuwa kazi zinaweza kupatikana humo, kujitolea, mawasiliano na vitu vingine vingi. Wachache ambao tuliweza kuwaandaa kibinafsi mwaka huo, waliingia mtaani kwa ujasiri na mpaka sasa wanafanya vizuri ila tukagundua pia kuwa wahitimu wengi hawapo tayari kuambiwa jambo na mtu wa mwaka wa chini yao na ili kukwepa tatizo hili, mbadala ulianza kutafutwa na ndiposa April 27 – 28, 2013 tukafanikiwa kuanzisha workshop moja iliyopewa jina la CCkwaCC workshop.

Maoni 1 :

  1. Ndugu wahitimu wa chuo kikuu cha DODOMA na pia wa wasio wahitimu ila mko tayari kujipatia ujuzi kipindi hichi cha likizo...

    Leo tunawaletea
    'envaya'

    ukiwa kwenye mtandao na ukaandika 'envaya' basi utakuwa kwenye page ya organization inayokusanya fursa zote za kujitolea, yaani, volunteering pote Tanzania na duniani kote, ni wewe tu kuchagua unataka kujitolea wapi.

    Tunawaombeni msikae nyumbani bure kipindi hichi cha likizo au wakati huu wa kujitafutia kazi.
    Asanteni na mtujulishe mmekwama ama mmefanikiwa wapi

    JibuFuta