Jumamosi, 29 Juni 2013

Toa maoni kuhusu mwongozo wa CCkwaCC


Utangulizi
Kutoka mwaka 2011/12, kulionekana upungufu mkubwa sana kwa wanafunzi (waliookoka) wanaohitimu kutojiandaa ama kutoandaliwa kuhitimu masomo yao na kuingia mtaani kwa ajili ya kuyakabili maisha baada ya chuo. Tuligundua watu wengi kutokuwa na maandalizi ya nyaraka muhimu kama vile CV na hata vyeti kutokuwa katika mpangilio unaokubalika. Pia wahitimu wengi mbali na kujua kutumia Internet kwa ajili ya kufanya kazi zao za darasani, imeonekana kuwa hapo ndio mwisho wao – hawajui kuwa kazi zinaweza kupatikana humo, kujitolea, mawasiliano na vitu vingine vingi. Wachache ambao tuliweza kuwaandaa kibinafsi mwaka huo, waliingia mtaani kwa ujasiri na mpaka sasa wanafanya vizuri ila tukagundua pia kuwa wahitimu wengi hawapo tayari kuambiwa jambo na mtu wa mwaka wa chini yao na ili kukwepa tatizo hili, mbadala ulianza kutafutwa na ndiposa April 27 – 28, 2013 tukafanikiwa kuanzisha workshop moja iliyopewa jina la CCkwaCC workshop.
Ilitokeaje: Katika kutafuta namna gani angalau wanaCASFETA wataweza kuwa na nuru watokapo kwenye maisha ya uanafunzi na kuyakabili maisha, Samson J. (PSPA) amekuwa akibadilishana mawazo na watu mbalimbali, ndipo siku moja uhakika wa upungufu mkubwa ulipodhihirika pale ambapo mashahidi wawili Kaaya G. (BAGE) na Kyando N. (BAGE) walipothibitisha kuwa hii hali ikiendelea kuachiwa hivi, hata ukombozi wa nchi yetu unaosemwa kila mara kuwa wanaCASFETA wataikomboa nchi utaendelea kuwa mgumu. Samson huwa anaweza kuthubutu kujaribisha jambo linaloonekana kuwa lingemfaidisha mtu mwingine huku yeye akiendelea kujipatia uzoevu na ujuzi ambao unakuja tu kama utamshirikisha mtu mwingine kile unachoona kuwa kisipokwepo kitasababisha upungufu unaopelekea uharibifu.
Jioni moja baada ya ibada (April 5, 2013) hapa Common Room ya Block 2, wahitimu wote waliombwa kubaki ili wauziwe maono, wote waliafiki na kamati ndogo kuundwa ikimhusisha Rajabu R. (BAPA), Leonard P. (IR), Charles G. (PHIL), Mfilinge M. (BAGE), Jonathan V. (EDM), Chisata D. (PPM&CD) na Mwinuka M. (DS). Hii ni kamati ambayo ilikutana rasmi kwa mara ya kwanza April 9, 2013 na kuidhinisha baadhi ya mambo.
Wakati huo huo, Samson kwakuwa ni mobilizer mzuri pia, alianza mchakato wa kukusanya emails za wahitimu na unakumbuka kuwa ndiye alikuwa mwasisi wa a centralized base ya taarifa za wanaCASFETA. Hivyo kazi ilikuwa rahisi zaidi.
Siku ya workshop ya kwanza, watu walifurahi sana na habari zikaenea kwani Samson mwenyewe aliShare ‘What to do from today on until you are employed’, Elisha D. (IR) akaShare ‘Forming business groups’, ‘Fund raising and donors finding’, ‘Time management’ na mwisho kwa siku hizo mbili za kwanza ni Mr. Magambo R. (Former UDOSO president na sasa ni Lecturer SJUT wakati huo huo akimiliki kampuni yake) aliShare ‘Financial skills’.
Lengo: siku ifike ambayo pasipo kuhurumiwa wala kupendelewa, mwanaCASFETA mmoja wetu astahili kuwa na wadhifa kwa ajili ya taifa letu – Dan 2:48
Kauli dira: kufaana sisi kwa sisi kwa kushirikishana ujuzi na taaluma mbalimbali hata kutokeza fursa ya haki – Dan 2:49
Mengi yapo ya kusema ila kwa waraka huu, tulitaka tu kuelezea malengo ya CCkwaCC Empowerment
1.       Kuwafundisha mwaka wa kwanza pindi tu wafikapo hapa chuo habari ya bum, matumizi na financial skills kwa ujumla wake ili
a.       Waweze kuwa imara wasichukuliwe na ulimbukeni wa kujishikia pesa zao wenyewe kwa mara ya kwanza na hivyo kutumia vibaya mpaka wanaishiwa njiani
b.      Kuweka mipango ya kununua laptop badala ya simu za gharama angalau ifikapo semester ya pili ya mwaka wa pili – tatizo kubwa linalowakabili wanaCASFETA hapa chuo wafikapo mwaka wa mwisho ili kuandaa nyaraka zao ni kutomiliki PC zao
c.       Kuwaelekeza washirika wetu waepuke kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi kama hawajapanga kuoa. Kwenye CCkwaCC tunasema ‘mwambie mtu unampenda kama tu upo tayari kuolewa naye/kumwoa leo na ya kuwa umeweka mpango kuwa upo tayari kuoa unapoenda kumwambia ama unapomkubalia kumpenda’. Tuwaambie washirika wetu wajitahidi kuweka ukaribu na wazazi wao hasa kwenye mambo haya ya kuoa na kuolewa. CCkwaCC huwa inashangaa mtoto wa kike/kiume anapokuwa kwenye mahusiano mwezi mzima bila ya mama/baba kujua. Kweli? Haikuandikwa wazazi ndiyo watu wa pekee wenye uwezo ku-Influence miaka yako ya kuishi? Je, wajua kuwa wewe kuolewa/kuoa ni kumwongeza mtoto mwingine kwenye familia ya wazazi wako? Iweje umlete mtoto mgeni ambaye hukuwahi hata siku moja kuwadokezea wazazi wako kuhusu kumkubali kwako? Siku Samson anaenda kuongea na huyu mwanamke mzuri leo, aliwaaga wazazi kuwa ‘naenda kumtongoza dada nanii akubali nimwoe’
d.      Kuelimisha wanachama wetu kuhusu optional courses, credits, supplementary,  disco, na mengine mengi ya kielimu hapa chuo – wengine wanaOpt kozi isiyo na mashiko
e.      Kuwapa mwaka wa kwanza walezi ambao ni mwaka wa pili/tatu/nne wa kozi zao
f.        Upatikanaji na utunzaji wa taarifa muhimu za mwaka wa kwanza kama vile room, block and phone number, degree program, full name, kijiji na wilaya atokako(nyumbani), mchungaji wake huko alikotoka na hapa akiwa chuo, na kama amebatizwa kwa maji mengi. Wapi anaenda wakati wa likizo hii na wapi atakwenda baada ya kuhitimu degree yake hapa chuo. Kwa ujumla ni kuwa, washirika wetu ni wale wanafunzi tu waliookoka na kubatizwa kwa maji mengi na wanaabudu kwenye makanisa ya kiPentekoste lakini yenye wachungaji wa mahali pamoja
g.       Muhimu sana: kuwahamasisha mwaka wa kwanza washirika wetu watumie ile likizo ya wiki mbili ya semester ya kwanza kuandaa CV ambayo itakuwa dira tayari kwa semester ya pili kulazimika wakajipatie maeneo ya kufanyia practical training for experience (kwa kujitolea BURE ama kulipwa ikitokea). Matatizo ni mengi kwa watu kutokuwa na ujuzi
h.      Kukazia usomaji kwa kutumia maarifa ili asiwepo mwanaCASFETA anayeshindwa kuwepo ibadani kisa anasoma sana , nafikiri kuna ushahidi wa baadhi ya watu walioDisko wakiwa washirika wanaCASFETA na walikuwa adimu ibadani na bado wamedisko wakati wale waaminifu bado wamefadhiliwa na Mungu.
i.         Kama zawadi hizi za kitaaluma huwa zinatolewa kwa haki, basi safari hii tunazitaka, tuna uwezo na tumejipanga na Bwana aridhie matakwa haya – ni ahadi yake pia
j.        Kuendeleza na kuhamasisha utumiaji wa computer katika kuangalia fursa za scholarships, kazi, volunteering, taarifa za kiujuzi, na kuwasiliana
k.       Elimu ya computer, hasa
                                                               i.      Emailing na matumizi ya soft ware mbalimbali – skype, viber, ….pc suite, Encarta, typing game, …. – watu wenye simu zenye internet sio wote wanatakiwa kununua modem, tuwaelimishe watu wetu
                                                             ii.      Ms word (HASA haya maeneo)
Spell checker; Referencing; Automatic table of content and cover page; Thesaurus; Pagination; Watermarking; Finding and replacing within a whole document; Insertions
                                                            iii.      Ms excel
                                                           iv.      Ms access na publisher
                                                             v.      Ms outlook
                                                           vi.      Ms power point
2.       Baada ya kuweka huo msingi kwa mwaka wa kwanza, sasa kazi inakuwa rahisi kwa miaka inayofuata kuwa ni mwendelezo tu kuweka nguvu kwenye
a.       Kuwaelimisha washirika wetu wazijue degree zao na kazi wanazopaswa/kuweza kufanya
b.      Kuwajengea uwezo waweze kujipatia marafiki maeneo yote kuanzia kwa lecturers ili iwe rahisi wakati wa kuwatafuta referees
c.       Leadership skills kwa mapana yake  - management vs administration
d.      Networking na watu mablimbali na mbinu hapa itakuwa ni kutembelea maeneo mbalimbali kama bungeni, workshops nyingi, kujiunga na organizations kama vile AIESEC, RestLess, BRAC, kuwa na email na kutumia kuwasiliana
e.      Kuwaelekeza washirika wetu wawe msaada makanisani mwao kwa wao kujitolea kutumia taaluma zao kuwaendeleza watu wengine. Tunataka iwe, kanisa lolote lenye mwanaCCkwaCC basi watu wote waliochini ya umri wa miaka 20 wajishugulishe kuwa na cheti cha form four kama ilitokea hawana ili waweze kujiendeleza kielimu
f.        Kuwahamasisha na kuwaelimisha washirika wetu wawe watu wanaotembea na mawazo ya kibiashara na waandike mawazo hayo huku wakiangaza nani wa kushirikiana naye kwenye biashara yenyewe – waazishe NGO, kampuni……. Tuwape elimu ya nini cha kuzingatia wakati wa kuwatafuta watu wa kufanyanao kazi – taaluma inayohusika, sababu ya mtu kuhusishwa, uwezo wa kuInfluence serikali/jamii, ……
g.       Kuelimisha washirika wetu waandike miandiko ya miradi kwa ajili ya vijiji vyao
h.      Business partnership – hisa na kuingia ubia na kampuni iliyotayari
i.         Uadilifu, kutunza muda na ubunifu (kujijengea ubora) kwenye kufanya haya mambo yote madogomadogo ya kawaida ambayo watu wengine huyafanya kwa kawaida
j.        Kuwajengea washirika wetu uwezo mkubwa wa Public Speaking
k.       Fursa ya uongozi CASFETA iwe ni a field of practice ya utumishi wa nchi
l.         Kujenga miundo ya lecturers wetu kukutana na washirika wetu via academic presentations
m.    Utambuzi wa vyuo nchi nzima na kugawa majukumu kwa wahitimu CCkwaCC iwe huko
n.      Kujiwekea akiba kubwa ya mtaji wa watu kwa kufanya mazuri huko kote tunakopita kuanzia mwaka wa kwanza – watu ni zaidi ya kuwa na hela nyingi za kufanyia utakacho
o.      Kuwakutanisha washirika wetu na makampuni mbalimbali kwa kuwaalika ama kuwapeleka wakatembelee huko VODACOM, MADINI, MANISPAA, TAMISEMI, …
p.      Kuelimisha namna ya kuandika ‘a current cover letter, resume, CV, application letter, scanning documents, attractive emails…… 
q.      Kuwalekeza washirika wetu watume CV zao mwanzoni mwa semester ya mwisho kwa mwaka wao wa masomo lakini wakielezea bayana siku yao ya kuhitimu chuo
r.        Kuweka bayana kuwa tunataka ¾ ya wanaCASFETA wawepo serikalini (watumishi waadilifu sana) lakini wakati uo huo kila mmoja akiwa na kitu anachokifanya nje ya ajira ya serikali – kuwepo serikalini ni fursa ya soko la biashara yako, fursa ya kufahamiana na watu, fursa ya security, fursa ya mtaji, ….

3.       Namna ya kufanya

a.       kuShare, sisi kwa sisi, yaani kila mmoja wetu mwenye kujua jambo fulani, ashirikishe
b.      kuwaalika watu nje ya chuo ili kushirikisha
c.       kufuatilia na kusimamia impacts ya kila sharing iliyotolewa – hasi kudhibitiwa na chanya kuendelezwa
d.      kuwa na mikutano ya mara kwa mara kwa ajili ya tathmini ya  nini kilijiri/kifuate
e.      mwanzoni mwa semester kabisa, kupanga na kujulisha kanisa kuhusu ratiba za CCkwaCC Empowerment ili ikitokea imegongana na ratiba ya kanisa, ihamishwe ya CCkwaCC na sio kuahirishwa – Setting objectives and action plans is a must in every year
f.        kufuatilia wahitimu wote wa mwaka uliopita kama wako wapi na wanafanya nini
g.       kuwaunganisha wahitimu wa mwaka huu na wale wa mwaka uliopita huko ‘mawilayani’ ama majumbani kwao
h.      kutunza kumbukumbu ya wahitimu na washirika wote kwenye hardcopy na softcopy – mfano upo kwenye nyaraka za Samson
i.         kuchagua uongozi kabla ya UE ya semester ya mwisho wa mwaka wa masomo
j.        kuwa na kamati ndogondogo kila inapohitajika – uwiano wa kozi utazingatiwa

4.       Waendelezaji wa CCkwaCC Empowerment hapa CHSS mwaka 2013/14
JINA KAMILI
SIMU
KOZI
YoS
SKULI
E MAIL
NYUMBANI
MARKO TIMOTHY
0762 187615
BASO
II
SS

Iramba
JUSTINE SAMSON
0768 338434
PSPA
-
SS
justinesamson34@yahoo.com
Monduli
MASSE DANIEL
0764 929637
BAGE
III
SS
massed89@gmail.com
Karagwe
JULIAN EMMANUEL
0765 257615
DS
III
SS


ANTHONY LEVINA
0714 992735
BBA
III
SH


OSWARD BADI
0766 241723
BCOM PLM
II
SH


FRANK KIGOYE
0712 315087
BCOM IB
II
SH


DANIEL THOBIAS
0765 294886
BA ENG
II
SH


ERASI EMMANUEL
0759 844364
Bsc CoEng
-
CIVE
myesierasi@yahoo.com

MATHIAS JAMES
0752 293434
LLB
II
SH


5.       Msimamo wetu

a.       Hata ijapokuwa tunafanya vitu ambavyo vinawezakumsaidia mtu aliye kiroho kuwa bora zaidi, hatuko kidini na hatufanyi chochote ambacho ni kinyume na maadili ya chama kinachotuweka pamoja kama wanafunzi tuwapo hapa chuo
b.      Wala hatuna na hatutaandaa ratiba zinazojitegemea nje ya chama chetu cha wanafunzi na kwahiyo, uongozi wa chama husika hapo tulipo unao uwezo wote kutuelekeza namna gani tuboreshe shughuli zetu na hata hivyo nakala ya mwongozo na ratiba zetu lazima katibu mkuu wa tawi letu awe nayo. Kiongozi mmoja mstaafu tawini ni mwanakamati wa tume ya kuendeleza CCkwaCC Empowerment – kamati kuu ya tawi kwa hiari ama kwa maombi yetu watamwidhinisha mmoja wao atakayekuwa mwanakamati

6.       Mwisho
Cloud Callout: Leo June 20 2013Mungu ibariki CASFETA ya Social Science – UDOM ili siku moja kupitia CCkwaCC Empowerment imtoe kiongozi mkubwa wa nchi hii, Mungu wabariki waasisi wa CCkwaCC, Mungu Ibariki Tanzania na ibariki Africa ambayo siku moja itakuwa ikiendesha CCkwaCC Empowerment kwa ajili ya kuwatoa wanafunzi bora waliookoka wenye elimu ya kutosha ya uraia kiasi cha kutofautisha siasa na ukombozi wa nchi zao. Siasa ina mbadala (pesa, nguvu, nafasi, umashuhuri n.k.) lakini ukombozi wa nchi ni wenyewe tu kuwa ni “wananchi watengwe mbali na wale maadui wakubwa wa nchi zetu ambao ni umaskini, ujinga na magonjwa”. Ni ujinga ndiyo unaoleta ubaguzi wa kidini, ni kiwango cha umaskini ndiyo unawafanya watu waandamane wiki nzima. Ni umaskini ndiyo unaoifanya serikali isijali maslahi ya wananchi wake na kupelekea wananchi waandamane kwa sababu viongozi wao wamejiwekeza kwenye kujali maslahi yao pekee
Imeandaliwa na Samson J. (PSPA) ______________ Mwasisi wa wazo
Na kusomwa/kuhaririwa na  wafuatao ambao walikuwa ni kamati ya kwanza kabisa ya CCkwaCC
1.       Up Ribbon: Leo June 21, 2013
Rajabu R. (BAPA)___________________,
2.       Leonard P. (IR)_____________________,
3.       Charles G. (PHIL)___________________,
4.       Mfilinge M. (BAGE)_________________,
5.       Jonathan V. (EDM)__________________,
6.       Chisata D. (PPM&CD)____________ ____na
7.       Mwinuka M. (DS) _____________________.
32-Point Star: Leo June 25, 2013Na kuridhiwa/kuidhinishwa na viongozi wetu wa CASFETA Social Science – UDOM 2012/13
1.       Mwenyekiti _______________ Julian Emmanuel (DS)
2.       Katibu __________________Fabian Bernard (PPM&CD)

Maoni 1 :

  1. Toa mawazo yako ili cckwacc iendelee kuwepo ikiwa bora na wewe ukiwa mdau mkuu ukiendelea kushiriki kuboresha

    JibuFuta