Alhamisi, 27 Juni 2013

Utakwepo DSM mnamo July 3, 2013?

Utakwepo DSM July 3, 2013? Soma hapa na ZINGATIA - SHIRIKI



KONGAMANO LA WAZI NA UZINDUZI WA MPANGO WA KULETA MATOKEO MAKUBWA SASA KWA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (Mbunge), anawaalika wadau wote wa Sekta ya Nishati na Madini kote nchini kwenye kongamano la wazi litakalofanyika siku ya Jumatano Julai 3, 2013 kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Mwenge Jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 11.00 jioni.

Mada kuu ni kujadili, kushauri na kutoa maoni juu ya miradi mikubwa ya kitaifa ya sekta ya nishati itakayotekelezwa na Wizara ya Nishati na Madini kwa kipindi cha miaka mitatu, Julai 2013 – Disemba 2015 ili kuliwezesha Taifa kufikia Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now).

Wadau wanaoalikwa ni pamoja na:

Mabenki washirika, Wakandarasi kwenye sekta ya Umeme, Wahandisi kutoka Taasisi na Vyuo Vikuu nchini, Mashirika ya Kiserikali na yasiyo ya kiserikali, Wawakilishi kutoka Makampuni mbalimbali, Migodi, Viwanda vikubwa na vidogo na wananchi wote kwa ujumla.

Hakuna kiingilio kwenye uzinduzi huo.

“Matokeo Makubwa sasa kwa maendeleo ya Mtanzania”

Imetolewa na:
Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini


Source: http://www.wavuti.com/4/previous/2.html#ixzz2XQLBAWfD




Pia soma kwa makini hapa chini kwa ajili ya June 28 (kesho) mpaka July 1, 2013 - Tunawaomba msikose jamani fursa kama hizi
 
Picture
Mfalme Mswati III wa Swaziland akiteremka kwenye ndege mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Mfalme ni miongoni mwa Wakuu wa Nchi na Serikali watakaohudhuria Mkutano wa Majadiliano kwa Manufaa ya Wote (Global 2013 Smart Partnership Dialogue) utakaofanyika hapa nchini kuanzia tarehe 28 Juni hadi 1 Julai, 2013.
Ndugu Watanzania,

Tujitokeze kumuunga mkono Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika Mkutano utakaofanyika Dar es Salaam kuanzia tarehe 28 Juni, 2013 hadi 01 Julai, 2013 maarufu kama SMART PARTNERSHIP INTERNATIONAL DIALOGUE.

Tuchangie hoja zitakazoleta mabadiliko na maendeleo ya taifa letu.

Tafadhali jiandikishe kupitia tovuti ya www.globaldialogue2013.go.tz

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
24/06/2013


Source: http://www.wavuti.com/4/previous/2.html#ixzz2XQN7KdNo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni