Jumatano, 26 Juni 2013

Leo ni siku ya ajabu social UDOM - CASFETA
Viongozi wetu wameitenga siku hii iongozwe na wahitimu lakini pia washuhudie na kuaga
Ni siku ambayo picha mbalimbali zatapigwa na kuwekwa kwenye blog yetu
itakuwa ni kumbukumbu ya kudumu
Washirika wetu wametangaziwa waje na wajiandaye kupiga picha za mwisho wa semester
maendeleo na uwekaji wa kumbukumbu ni kipaumbele kikuu sasa hapa Social maana kuna baraka zinakuja mbele ambazo kama kumbukumbu za nyuma hazipo, hutaweza kumshukuru Mungu kwa Uzito unaopaswa
Tunategemea pia kuwa kuna kiongozi mkubwa wa nchi hii atatokea Social CASFETA so siku ikifika ni kufungua tu nyaraka na kusema huyu ndiye

Tunaomba ushirikiano wenu, maboresho, mapendekezo, habari, .......

Makampuni muda sio mrefu utayaona yanajitangaza hapa na kuanza kuwaajiri washirika wetu

Nafasi za field zitakuwa zinapatikana hapa kwa makampuni kutujulisha fursa zilizopo

Matokeo ya workshops mbalimbali zitakazo endeshwa na CCkwaCC zitawekwa hapa

Matangazo ya kazi za kitaifa na binafsi zitakuwa hapa tukishirikiana na jobstanzania, tume ya ajira, ajirablog, ........
kila shahada iliyoko hapa chuo Kikuu cha Dodoma kitaelezewa na kuuzwa sokoni mbele ya makampuni

Contacts za wahitimu na mahali walipo huko waendako na watakakokuwa zitatunzwa
Ni kazi endelevu maadam Social ipo na UDOM ipo na CASFETA inawaweka vijana pamoja
Tujitokeze kutembelea hii blog kila mara kuna kitu kipya, asanteni

Maoni 4 :

  1. Aisee!
    Shuhuda!
    Wosia!
    Wafuatao waliongea mambo mazito na shuhuda za kazi:
    Leonard (IR), Samson (PSPA), Namala (PABA), Emelda (BAPA), Dominico (BAPA), Lilian (PABA), Mary(DS), Recho (BAPA), Upendo (BAPA), Debora (BAPA), Farida (IR), Senfros (DS), Zaituni (PSPA), Elisha (IR), Rahabu (BAPA), Makumba (IR), Sang'udi (LLB), Seth (BAPA), Joel (BAPA), Domina (IR), Bresta (IR), Jofu (PHIL), Emmy (BAPA), Damian (BAPA), Mena (BAPA)
    Watu wamemshukuru sana Mungu, watu wameaga, imekuwa nzuri sana, philosophers wamerejewa, wameongoza ibada, kupiga picha za pamoja, picha za vikundi, kikozi, viongozi, marafiki, aisee hatuna namna ya kukuelezea uliyekosa kuwepo

    JibuFuta
    Majibu
    1. Raheli Ndalusanye (BAPA) hakusahaulika, ndiye aliyekuwa akiongoza matukio yote haya kwenda vyema

      Futa
    2. Hapana, Watu wa degree ya pili walikwepo na wao wameaga
      Yupo Stephen Simba (MA-Ling), na Emanuel Mayaya (MBA) - watu wa Mungu wameacha wosia

      Futa
  2. Kwakweli ilikuwa siku nzuri sana yakutosahaulika...asantee uongozi kwa heshima mliotupa Mungu awabariki!!

    JibuFuta